Matokeo ya COVID-19

AngloGold Ashanti inatambua kwamba wadau wetu wote wana maslahi ya moja kwa moja katika namna ambavyo sisi, kama Kampuni, tunajiweka tayari na kushughulikia tatizo la COVID-19 katika migodi yetu na jamii zetu. Tatizo hili limeleta changamoto ambayo haijawahi kutokea kabla, na linachukua sura mpya kila siku na kwa haraka, na hivyo tunapaswa pia kuchukua hatua za haraka katika kupanga na kutekeleza mipango ya kulishughulikia. Tukiongozwa na Tunu na ahadi yetu ya kulinda afya za wafanyakazi wetu na jamii zinazotuzunguka, tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha shughuli za uzalishaji zinaendelea

Ujumbe kutoka kwa Kelvin

Kelvin Dushnisky
Ofisa Mkuu Mtendaji

Wenzangu,

Bila shaka mmeona vichwa vingi vya habari kuhusu virusi vya Korona, COVID-19 na mmeona hatua ambazo zimechukulia na serikali nyingi duniani kote kudhibiti kusambaa kwake. Huku ninapofahamu wasiwasi mkubwa ambao wengi wenu mnao juu ya afya na maslahi yenu na yale ya watu mnaowapenda, huu ni wakati wa kutulia na kuchukua hatua ya maamuzi dhahiri -- kibinafsi na kwa pamoja -- kupunguza athari ya mkurupuko huu na kuzuia kusambaa kwa ugonjwa.

Kama biashara, tayari tumechukua hatua kuhusu suala hili na tunaongozwa na kipaumbele chetu cha kwanza, ambacho ni kuhakikisha usalama na afya yako.

Tumeanzisha makundi mawili ambayo yanafanya kazi kwa bidii ili kulinda watu na biashara yetu. Kwanza, Kikosi cha Kazi cha COVID-19 ambacho kinashughulika na njia ya kimkakati ya kudhibiti mkurupuko huu na athari yake kwa watu na biashara yetu. Na pili, Kamati ya Hali ya Hatari ya COVID-19 ambayo inalenga kuhakikisha kuwa suluhusu hizi zinatekelezwa haraka na kwa ufanisi kadri iwezekanavyo kwa kila sehemu ya kazi. Makundi haya yanahakikisha kuwa tunachukua hatua kwa haraka na kujifunza kutokana na uzoefu wa kila mmoja wetu.

Tayari suluhu zimewekwa katika sehemu nyingi za kazi yetu -- na hivi karibuni tutafikia sehemu zingine -- kuongeza shughuli za uchunguzi kulingana na safari, dalili za ugonjwa na wale walio na halijoto la juu la mwili. Hii itahakikisha kuwa watu ambao wanaweza kuwa wagonjwa wanatambuliwa mapema, wanapewa matibabu wanayohitaji haraka iwezekanavyo na hawasababishi hatari kwa wengine.

Unaweza kutarajia kupata mawasiliano ya mara kwa mara kutoka kwetu tunapokabiliana na changamoto hii, ambayo yatakuwa ni pamoja na mwongozo kutoka kwa Rasilimali-Watu za Kundi na kutoka kwa sehemu mahususi panapohitajika.

HALI YA SASA

Ingawaje Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeainisha kusambaa kwa COVID-19 kama maradhi yaliyoenea ulimwenguni kote ni muhimu kukumbuka kuwa:

 • Asilimia ndogo mno ya watu wazima wenye afya nzuri walipata matatizo hatari ya kiafya;
 • Wazee na wale wenye mfumo dhaifu wa kinga ya mwili au wenye magonjwa sugu, ndio walio katika hatari kubwa zaidi;
 • Kwa sasa hakuna chanjo au matibabu mahususi, lakini tunahimizwa kuwa idadi kubwa ya wale walioathiriwa hupata nafuu dhidi ya virusi.

Kulingana na kusambaa kwa COVID-19 na matamanio yetu ya kuchangia katika kudhitibi virusi, sasa AngloGold Ashanti imeanzisha baadhi ya itifaki ambazo zinapaswa kutumiwa katika kampuni.

TUMIA BUSARA

Ikiwa una dalili zinazofanana na zile za mafua, umechunguzwa na kupatikana kuwa una mafua, umepimwa na kupatikana kuwa una COVID-19 (virusi vya Korona) au umetangamana na mtu aliye na virusi, salia nyumbani na uwasiliane na daktari wako.

Ikiwa unashuku kuwa umetangamana na mtu aliye na virusi, lakini hauonyeshi dalili, mwarifu msimamizi wako mara moja.

KUSAFIRI

 • Safari za kimataifa za kibiashara zisizo za muhimu zimesitishwa kwa siku 30 zijazo, wakati ambapo kizuizi hiki kitakaguliwa.
 • Safari za kimataifa za kibiashara zenye umuhimu zinahitaji idhini ya EVP / COO yako au huduma zao mbadala zilizotengwa.
 • Mbinu ya kusafiri ya watu wasio ishi katika nchi zao na familia zao itashughulikiwa katika kiwango cha sehemu ya kazi, kulingana na muktadha wa kila nchi. Usafari huu utaidhinishwa na huduma mbadala za COO zilizotengwa.
 • Mwarifu msimamizi wako kuhusu safari ya hivi majuzi na uliyoipanga, bila kujali iwapo safari ni ya kibiashara au ya sababu za kibinafsi.
 • Hifadhi nafasi za safari zote za kibiashara na mabadiliko ya safari kupitia vituo vilivyoidhinishwa na AGA. Hakuna hali za kipekee.

Wasafiri wanahimizwa kuwa makini zaidi na kufuata tahadhari hizi:

 • Ikiwa unajihisi mgonjwa, tafadhali ripoti mara moja kwa mtoa huduma za afya au wafanyakazi wa ndege;
 • Usisalimiane kwa mikono/kukumbatiana;
 • Zingatia zaidi usafi wa chakula na wa kibinafsi;
 • Safisha mikono mara kwa mara, hasa baada ya kugusa majimaji yanayotoka kinywani au puani. Usafi wa mikono unajumuisha kusafisha mikono kwa sabuni na maji au na kisafishaji cha mikono kilichotengenezwa kutokana na pombe. Visafishaji vya mikono vilivyotengenezwa kutokana na pombe vinapendelewa ikiwa mikono haina uchafu unaoonekana; osha mikono kwa sabuni na maji ikiwa ina uchafu unaoonekana;
 • Funika pua na mdomo kwa kiwiko cha mkono au karatasi shashi; unapokohoa au kupiga chafya na uitupe mara moja na usafishe mikono;
 • Usiguse mdomo au pua lako;
 • Usikaribiane na watu wagonjwa hasa wale walio na dalili za matatizo ya kupumua na homa;
 • Usiende kwenye masokoni na kukaribiana na wanyama wagonjwa au waliokufa ikiwa utasafiri kwenda katika maeneo yalioathirika;
 • Hakikisha kuwa unakula bidhaa za nyama zilizopikwa vizuri na usile bidhaa mbichi.

ITIFAKI ZA MAHALI PA KAZI

Wafanyakazi na wakandarasi wote wanaofanya kazi katika AGA, wanapaswa kufuata mwongozo ufuatao ili kulinda afya na usalama wa wafanyakazi na wakandarasi wetu na kudumisha kuendelea kwa kazi hadi ilani zaidi itakapotolewa:

 • Punguza idadi ya wageni wanaokuja mahali pa kazi kadri iwezekanavyo.
 • Hakikisha kuwa wageni wote wanaweka sahihi kwenye kitabu cha wageni kilicho langoni na watoe maelezo ya mawasiliano (simu, barua pepe, maelezo ya safari za kimataifa katika wiki mbili zilizopita). Ni lazima mgeni yeyote atii masharti ya kuchunguzwa kiafya na itifaki za usimamizi ambazo zinatumika kwa wafanyakazi wa AGA.
 • Tumia simu za Skype, mikutano ya video za simu au njia nyingine za kufanya biashara bila kutegemea mikutano ya ana kwa ana.
 • Kuwa na kompyuta yako ya kupakata kila wakati nyumbani kwako na vifaa vingine vya kielektroniki au karatasi utakazohitaji iwapo ofisi itafungwa au vinginevyo uelekezwe kufanyia kazi nyumbani.
 • Mwongozo wa ziada kwa maeneo mahususi ya kazi unaweza kutolewa kivyake na usimamizi wa sehemu ya kazi jinsi inavyohitajika.

Zingatia usafi katika mahali pa kazi:

 • Mfanyakazi yeyote aliye na dalili kama za mafua anapaswa kupokea huduma ya matibabu haraka iwezekanavyo na arejee tu kazini baada ya dalili kutoweka kabisa;
 • Dumisha usafi wa mahali pako pa kazi na mjisafishe wote katika maeneo ya kawaida;
 • Osha mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji;
 • Tumia kisafishaji cha mikono ikiwa kituo cha kuoshea mikono hakipatikani;
 • Tumi karatasi shashi au ufunika mdomo wako kwa mkono wako unapokohoa au kupiga chafya;
 • Usikaribiane na watu wengine, ikiwa ni pamoja na kusalimiana kwa mikono; na

Ikiwa umepimwa na kupatikana kuwa una COVID-19:

 • Mwarifu meneja na/au HR wako mara moja na uwasiliane nao mara kwa mara kadri uwezavyo kuhusiana na hali yako ya afya;
 • Unahitaji kuwa na dokezo la daktari la kukuruhusu urejee kazini.

Tunafahamu kuwa kuna maswali mengi. Tunakuhimiza uwasiliane na msimamizi wako, kliniki au mwakilishi wako wa Rasilimali-Watu ikiwa una maswali yoyote. Tutaendelea kutii sera zetu na sheria za mahali tulipo zinazosimamia ofisi na sehemu zetu za kazi.

Kwa kutamatisha, ningependa kuwakumbusha kwamba tunapokuwa katika nyakati za hali ya hatari, huonekana kuwa hazitawahi kupita. Bila shaka, nyakati hizi hupita, lakini kwa sasa, ni lazima tufanye kazi kwa pamoja na tuwe waangalifu.

Shukrani za ukarimu,

Kelvin Dushnisky
Ofisa Mkuu Mtendaji

Taarifa hii fupi imesambazwa kwa: watumiaji wote wa AngloGold Ashanti ulimwenguni kote

Por razones administrativas este comunicado fue enviado simultáneamente a todas las operaciones de AngloGold Ashanti en el mundo, razón por la cual el mismo está redactado en idioma inglés. En las próximas horas, en caso de corresponder, se enviará una versión traducida al español.

Por questões estratégicas, este comunicado foi enviado simultaneamente a todas as operações da empresa no mundo e por isso está em inglês. Nas próximas horas, você voltará a recebê-lo, porém já traduzido para o português.

Pour des raisons administratives, ce dossier a été envoyé en Anglais et simultanément à toutes les opérations d'AngloGold Ashanti dans le monde. Pour une traduction en français, et si vous avez des questions, contactez svp votre équipe de communication locale.

Kelvin Dushnisky Ofisa Mkuu Mtendaji

More information on:

https://www.who.int/emergencies/diseases/novel-coronavirus-2019

https://pandemic.internationalsos.com/2019-ncov

 

Taarifa mpya kabisa

29 January 2020

Global brief: Raising awareness of the novel Coronavirus outbreak in China

NJIA ZA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA MGODI KUJIKINGA

Kampuni ya Uchimbaji wa Dhahabu Geita (GGML) Yawaandaa Wafanyakazi na Wakandarasi Wake Juu ya Namna ya Kujikinga na Virusi vya Korona (COVID -19)

Katika juhudi za kuhakikisha kwamba wafanyakazi na wakandarasi wanafanya kazi katika mazingira salama, uongozi wa GGML umechukua hatua madhubuti za kuwakinga wafanyakazi wake dhidi ya maambukizi ya janga la COVID-19.

Juhudi mbalimbali zimefanywa na Kampuni kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo.

Vifaa vya kunawia mikono vimewekwa katika maeneo yote ya kuingilia na wafanyakazi wote wanapaswa kuosha mikono yao mara kwa mara kama inavyoelekezwa katika miongozo ya Afya dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Wafanyakazi wa kitengo cha Ulinzi wanachukua tahadhali za ziada wanapoingia mgodini, ambazo hujumuisha pia kuvaa barakoa na glovu wanapofanya ukaguzi, na pia wanapofanya upimaji wa joto la mwili kwa wafanyakazi, wakandarasi na wadau wengine kabla hawajaruhusiwa kuingia ndani ya mgodi.

Vipeperushi vya kuelimisha watu kuhusu COVID-19 vimebandikwa katika mbao za matangazo, vikiwa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuwawezesha wafanyakazi kuelewa ujumbe uliolengwa kuwafikia.

Tahadhali zingine zilizochukuliwa na Kampuni ni pamoja na kuondoa misongamano kwa kupunguza idadi ya watu na idadi ya mikutano, matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama vile “Skype Business”, kuwapanga vizuri watumiaji wa vyumba vya kubadilishia nguo na kupunguza idadi ya watu wanaoingia katika bwao la chakula kwa asilimia thelathini (30%).

Bw. Wallace Bude akichukua tahadhali dhidi ya virusi vya Korona kwa kunawa mikono kwa sabuni na maji-tiririka kwenye lango la kuingilia mgodini.
Ujenzi wa Kituo Maalum cha Kutenga Watu wanaohisiwa Kuathiriwa na COVID-19 katika Mgodi wa Geita ukiwa unaendelea.
Mfanyakazi wa Mkandarasi, Bi. Neema Molel akinawa mikono kwa sabuni na maji-tiririka kama sehemu ya juhudi za kujikinga na virusi vya Korona.
Mfanyakazi wa kitengo cha Ulinzi, Bw. Wilson Mapambano akipima joto la mtu anayetaka kuingia ndani ya eneo la mgodi.